Timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wachezaji saba upande wa Shujaa, imepoteza mchuano wa pili wa kundi C alama 12-7, dhidi ya Uingereza .
Matokeo haya yanaongeza shinikizo kwa Shujaa ambao hawana budi kuwashinda Ufaransa katika mchuano wa mwisho mapema kesho, ili kufuzu kwa robo fainali ya kombe kuu kwa mara ya kwanza msimu huu.
Kenya ilianza vyema ikiinyuka Uhispania pointi 19 kwa nunge mapema leo.