Kenya yaikaribisha Lithuania kufungua ubalozi wake Nairobi

Mudavadi alisema Lithuania itafaidika pakubwa na fursa zilizopo Afrika Mashariki na katika soko huru la kibiashara Afrika (AfCFTA).

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa mambo ya Nje wa Kenya Musalia Mudavadi ashiriki mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Lithuania Vidmantas Verbickas, Jijini Nairobi.

Kenya imeipongeza Lithuania huku inapojiandaa kuchukua wadhifa wa Rais wa Muungano wa Ulaya, huku ikilenga kuimarisha ushirikiano wake na taifa hilo.

Akizungumza alipokuwa mwenyeji wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Lithuania Vidmantas Verbickas afisini mwake leo Jumatano, Mudavadi alisema mazungumzo kati yao yaliangazia njia za kuboresha mbinu za kutoa fursa mpya za ushirikiano, huku akitoa wito kwa taifa hilo kufungua ubalozi wake Jijini Nairobi.

Mudavadi alisema Lithuania itafaidika pakubwa na fursa zilizopo Afrika Mashariki na katika soko huru la kibiashara Afrika (AfCFTA).

“Biashara yetu inapoimarika, natoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua dhabiti kuzipa pengo la kibiashara ikiwa ni pamoja na kuharakisha mikataba kuhusu biashara, ushirikiano wa uhamasishaji kuwasaidia wakulima na wanaouza bidhaa nje ya nchi ili kuafikia viwango vya soko la Bara Ulaya,” alisema Mudavadi.

Kulingana na Mudavadi aliyepia Mkuu wa Mawaziri, alidokeza kuwa Kenya inabuni ushirikiano Imara na Lithuania, uliojikita katika biashara, uvumbuzi na ugawanaji wa fursa sawa.

Share This Article