Kenya yaicharanga Ushelisheli 5-0 Kasarani

Nahodha Michael Olunga and Ryan Ogam walibusu nyavu mara mbili kila mmoja naye Collins Sichenje, akaongeza moja.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, imesajili ushindi wa pili wa kundi F kufuzu kwa Kombe la Dunia baada ya kuwacharaza Ushelisheli mabao 5-0, katika mchuano uliosakatwa Jumanne jioni katika uwanja wa Kasarani.

Nahodha Michael Olunga and Ryan Ogam walibusu nyavu mara mbili kila mmoja naye Collins Sichenje, akaongeza moja.

Ushindi huo ulikuwa wa pili kwa Harambee Stars katika kundi hilo huku wakichupa hadi nafasi ya nne.

Hata hivyo, Kenya haina uwezo wa kufuzu moja kwa moja au katika nafasi ya pili ili kushiriki mchujo.

Kenya watazuru Burundi mwezi ujao kwa mechi ya mzunguko wa 9.

Website |  + posts
Share This Article