Serikali ya Kenya imetangaza kufunga ubalozi wake Jijini Bern nchini Uswizi, kama sehemu ya mpango wa kufanyia mabadiliko balozi zake kote duniani.
Kulingana na taarifa ya ubalozi huo, Wakenya na wateja wengine ambao wamefahamishwa kuwa stakabadhi zao ziko tayari, wameshauriwa kuzichukua kufikia Novemba 30, 2026, ukisema utawafamahisha ni lini waliotuma maombi kuanzia Novemba 1, 2026, watachukua stakabadhi zao .
“Waliotuma maombi wameagizwa kuwasilisha vitambulisho vyao halali pamoja na risiti za kutuma maombi, wanapowasili kuchukua stakabadhi zao,” ilisema taarifa ya ubalozi huo.
Katibu wa idara ya Mambo ya Nje Korir Sing’Oei, alisema hatua hiyo sehemu ya mabadiliko kwenye balozi za Kenya kote ulimwenguni, yanayojumuisha kufungwa na kufunguliwa kwa balozi mpya.
“Wakenya wataendelea kupokea huduma bora licha ya mabadiliko hayo,” alisema Sing’Oei kupitia ujumbe kwenye ukurasa wa X.