Blue Samurai ya Japani yaikomoa Tunisia, yaitema nje ya Kombe la Dunia

Ushindi huo ndio mkubwa zaidi kwa Japani kusajili katika historia yao ya Kombe la Dunia, matokeo yaliyoweka hai matumaini yao ya kufuzu kwa raundi ya 32 bora.

Dismas Otuke
1 Min Read

Japani ilisajili ushindi mkubwa wa mabao 4-0 katika pambano la kundi F lililosakatwa mapame Jumapili mjini Monterrey, Mexico.

Daichi Kamada alifungua karamu ya mabao kwa Blue Samurai katika dakika ya 4, kabla ya Ayase Ueda kuongeza pili dakika ya 31, na Wajapani wakiongoza 2-0 kufikia mapumziko.

Kipindi cha pili hali ilikuwa iyo hiyo, Junya Ito akiongeza bao la tatu la dakika ya 69,naye Ayase Ueda, akaongeza la pili zikisalia dakika saba kipenga cha mwisho kipulizwe.

Ushindi huo ndio mkubwa zaidi kwa Japani kusajili katika historia yao ya Kombe la Dunia, matokeo yaliyoweka hai matumaini yao ya kufuzu kwa raundi ya 32 bora.

Hata hivyo, Carthage Eagles waliocheza mechi  hiyo chini ya kocha mpya Herve Renard, walibanduliwa nje ya fainali hizo baada ya kupoteza mechi ya pili mtawalia .

Japani ni wa pili kundini humo kwa alama 4 sawa na Uholanzi huku  Uswidi, wakiwa na alama 3 nao Tunisia wanaburura mkia bila alama.

Share This Article