Ujerumani ilikuwa timu ya tatu kujikatia tiketi kwa awamu ya 32 bora katika Kombe la Dunia baada ya kutoka nyuma na kuilaza Ivory Coast mabao 2-1 katika mchuano wa kundi E uliosakatwa Jumamosi usiku mjini Toronto, Canada.
Ivory almaarufu The Elephants walichukua uongozi kunako dakika ya 30 kupitia kwa nahodha Frankie Kesie huku magoli mawili ya Wajerumani yakikataliwa.
Nguvu mpya Deniz Undav aliwakomboa Ujerumani kwa bao la dakika ya 68 kabla ya kuongeza la pili dakika ya 94.
Kufuatia ushindi huo, Ujerumani wamejihakikishia kuongoza kundi hilo kwa pointi 6 wakifuatwa na Ivory Coast kwa pointi 3.
Ecuador na Curacao waliotoka sare tasa mapema Jumapili wana alama moja kila moja.