Simba wa Atlas wanusia raundi ya 32 bora baada ya kuibwaga Scotland

Atlas Lions watarejea uwanjani kwa mechi ya mwisho ya makundi dhidi ya Haiti Juni 25, wakati Brazil, wakimaliza udhia dhidi ya Scotland.

Dismas Otuke
1 Min Read

Morocco almaarufu Atlas Lions wamenusia kufuzu kwa raundi ya 32 bora ya Kombe la Dunia baada ya kuwalaza Scotland, bao moja kwa bila katika mechi ya kundi C, iliyosatwa mapema Jumamosi mjini Boston,Marekani.

Kiungo wa PSV, Ismael Saibiri,alipachika bao la dakika ya 2 baada ya kupokea pasi ya Brahim Diaz, na kulinda uongozi huo hadi kipenga cha mwisho.

Morocco waliomaliza katika nafasi ya nne mwaka 2022 wanaongoza kundi hilo kwa alama 4 sawa na Brazil, iliyowacharaza Haiti mabao 3-0 mjini Seatle.

Atlas Lions watarejea uwanjani kwa mechi ya mwisho ya makundi dhidi ya Haiti Juni 25, wakati Brazil wakimaliza udhia dhidi ya Scotland.

Wakati uo huo Uturuki na Haiti zimeyaaga mashindano hayo baada ya kupoteza mechi mbili za ufunguzi.

Share This Article