Je, uamuzi wa rufaa ya Hakimi wakati wa Kombe la Dunia unalenga kumvuruga?

Hakimi alicheza dakika zote 90 za ushindi huo ambapo kwa sasa wamecheza mechi 39 bila kushindwa.

Dismas Otuke
2 Min Read

Hatua ya Mahakama ya Rufaa ya Ufaransa kutoa uamuzi wa rufaa aliyowasilisha nahodha wa Morocco Achraf Hakimi, huenda iwe njama ya kumvuruga na kuathiri mchezo wake katika mashindano ya Kombe la Dunia yanayoendelea nchini Marekani, Mexico na Canada.

Mahakama iliamuru Ijumaa iliyopita kuwa Hakimi anapaswa kufunguliwa mashtaka kwa madai ya ubakaji.

Hakimi alikuwa amekata rufaa kutaka kesi hiyo itupiliwe mbali kwa kukosa ushahidi wa kutosha.

Hata hivyo, swali la kujiuliza ni mbona uamuzi wa kesi yake ya rufaa uafanywe saa chache kabla ya mlinzi huyo kuiongoza timu yake kwa mechi muhimu ya Kombe la Dunia dhidi ya Scotland?

Pengine mahakama ilikuwa na nia ya kumwathiri Hakimi kisaikolojia na wachezaji wenzake katika mechi hiyo.

Je, ingekuwa bora huo kutolewa baada yake kushiriki Kombe la Dunia?

Akizungumzia uamuzi wa kufunguliwa mashataka, Hakimi kupitia ukurasa wake wa X alisema,

“Leo hii taarifa ambayo sio yangu inasimuliwa na kuhatarisha familia yangu, maisha yangu, na zaidi ya yote ukweli. Wakati mwingine mimi huona kama nimekuwa mlengwa rahism,”alisema Hakimi.

Mchezaji huyo anaonekana kutotetereka wala kutishwa na uamuzi huo akisema yuko tayari kujibu kesi hiyo baada ya kusema,

“Nimekuwa nikisubiri kuanza kwa kesi hii tangu siku ya kwanza. Na sasa naisubiria. Hatimaye, nitapata fursa ya kuongea.”

Hakimi aliye na umri wa miaka 23 alishtakiwa mwezi Machi mwaka 2023 kwa madai ya ubakaji na kukanusha kutekeleza uovu huo.

Jambao lingine linalowafanya wengi kutilia shaka ni mbona mahakama itoe uamuzi wa kuendelea kwa kesi bila kutangaza tarehe ambayo kesi hiyo inapaswa kuanza kusikilizwa? Kunao wanaokisia kuwa pengine uamuzi huo ulifikiwa haraka bila mpangilio.

Mechi hiyo ilikuwa na umuhimu mkubwa kwani ushindi wa Morocco wa bao moja kwa bila dhidi ya Scotland umewaweka Atlas Lions katika nafasi bora ya kuongoza kundi C.

Hakimi alicheza dakika zote 90 za ushindi huo ambapo kwa sasa wamecheza mechi 39 bila kushindwa.

Morocco huenda waongoze kundi hilo endapo watapata ushindi mkubwa katika mechi ya mwisho dhidi ya Haiti Jumatano ijayo.

Share This Article