Barcelona ndio washindi wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, kwa wanawake,baada ya kuwachachafya Olympic Lyon, magoli 4-0, katika fainali iliyopigwa Jumamosi mjini Oslo -Norway.
Iliwabidi Barca kusubiri hadi kipindi cha pili kabla ya mshambulizi Ewa Pajor, kuwaweka uongozini katika dakika ya 55 na kuongeza la pili dakika ya 69, naye Salma Paralluelo, akacheka na nyavu mara mbili.
Barcelona wamenyakua mataji yote manne ya nyumbani na ugenini na manne ya Ligi ya Mabingwa katika misimu sita iliyopita.