Mfalme Mohammed wa sita wa Morocco ,amewaachilia huru mashabiki wa Senegal, waliofungwa gerezani nchini humo kwa makosa ya kuzua vurumai wakati wa fainali ya Kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) Januari 18 mwaka huu.
Kulingana na taarifa ya Mahakama ya Morocco,Mfalme Mohammed wa sita, amewaachilia huru mashabiki hao kwa misingi ya kibinadamu.
Mahakama ya Morocco, iliwahukumu mashabiki 18 wa Senegal, vifungo vya gerezani kati ya miezi mitatu na mwaka mmoja .
Mashabiki watatu waliachiliwa huru mwezi Aprili mwaka huu, baada ya kukamilisha vifungo vya miezi mitatu.
Kwa mjibu wa wakili wa mashabiki hao Patrick Kabou,15 hao waliachiliwa huru Jumamosi.