Mahakama moja ya kijeshi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,DRC, imewahukumu wanajeshi 66 kifo, baada ya kupatikana na makosa matatu, ikiwa ni pamoja na kuwa waoga.
Wanajeshi zaidi ya 70 walihukumiwa katika mahakama ya kijeshi ya goma, ambapo wanajeshi wanne waliachiliwa huru na mmoja akahukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani.
Wanajeshi hao wa kikosi cha 3415, walikamatwa Oktoba 20, 2026 katika eneo la Walikale kwa makosa ya kukaidi amri na uwoga walipokuwa wakikabiliana na maadui.
Kulingana na jeshi la DRC, kesi hiyo inalenga kuimarisha nidhamu miongoni mwa wanajeshi wake wakati wanapokabiliana na maadui mashariki mwa nchi hiyo.
Mnamo mwezi Oktoba, mahakama moja ya kijeshi nchini DRC iliwahukumu kifo wanajeshi 27 walipoondoka kwenye mstari wa mbele walipokuwa wakikabiliana na wanamgambo ya AFC/M23.
Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu nchini humo, yamepinga vikali adhabu hiyo ya kifo, licha ya kwamba hadi kufikia sasa hakuna hukumu rasmi ya kifo ambayo imetekelezwa.