Polisi wamkamata mshukiwa wa ulanguzi wa mihadarati Mombasa

Mshukiwa huyo anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Jomvu, akisubiri kufikishwa mahakamani.

Tom Mathinji
1 Min Read
Mshukiwa wa ulanguzi wa mihadarati akamatwa Mombasa.

Maafisa wa Polisi kutoka kituo cha polisi cha kaunti ndogo ya  Jomvu, wamemkamata mshukiwa wa ulanguzi wa mihadarati akiwa na vipande 20 vya dawa za kulevya, kwenye operesheni iliyotekelezwa katika eneo la Kisurini, kaunti ya Mombasa.

Mshukiwa huyo anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Jomvu, akisubiri kufikishwa mahakamani, huku mihadarati hiyo iliyonaswa ikihifadhiwa kama ushahidi.

Hatua hiyo inajiri saa chache baada ya maafisa wa polisi kaunti ya Mombasa kunasa kilo 454 za methamphetamine, zenye thamani ya shilingi 3.6 , ambapo washukiwa watatu walikamatwa kwenye operesheni ya kijasusi iliyotekelezwa na maafisa hao.

Huduma ya Taifa ya Polisi, imewapongeza wananchi kwa ushirikiano katika utoaji habari ambao ni muhimu kwenye msako unaoendelea kote nchini dhidi ya ulanguzi wa utumizi wa dawa za kulevya.

“Tunatoa wito kwa kila mmoja kuripoti visa vyovyote vya kutiliwa shaka katika kituo cha polisi kilicho karibu,” ilisema Huduma ya Taifa ya Polisi kwenye taarifa.

TAGGED:
Share This Article