Kenya imeboresha mazingira yake ya kibiashara na kisheria ili kuhakikisha uwekezaji na haki ya kumiliki mali vinalindwa ipasavyo.
“Hatua hizi za kimkakati hatimaye zitaifanya Kenya kuwa moja ya nchi zinazoongoza kwa uwekekezaji duniani.”
Rais William Ruto alitoa kauli hizo wakati wa mkutano wa wawekezaji wa Indonesia uliofanyika katika Ikulu ya Nairobi jana Alhamisi jioni.
Ujumbe wa Indonesia uliongozwa na Waziri wa Masuala ya Majini na Uwekezaji Luhut Binsar Pandjaitan.
Ujumbe huo upo nchini kutafuta fursa za uwekezaji katika sekta za mafuta na gesi, mafuta ya mawese, kilimo na madini miongoni mwa sekta zingine.