Kenya ilizindua utoaji chanjo ya Lenacapavir, ambayo inatoa kinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Chanjo hiyo ambayo itatolewa mara mbili kwa mwaka na ambayo inatolewa kwa mara ya kwanza humu nchini, itatoa kinga ya maambukizi ya virusi vya HIV kwa watakaodungwa sindano.
Uzinduzi wa chanjo hiyo uliandaliwa siku ya Alhamisi mtaani Dagoreti, jijini Nairobi, ukiongozwa na Waziri wa Afya Aden Duale.
Hatua hiyo inalenga kupunguza maambukizi mapya ya UKIMWI huku Kenya ikiwa na idadi ya watu milioni 1.4 wanaogua ugonjwa huo.
Chanjo ya Lenacapavir inatolewa bure bila malipo kwenye vituo vyote vya umma kote nchini, hususan kaunti au sehemu zenye maambukizi mengi.
Serikali ya Kenya ilipokea dozi 21,000 za chanjo dhidi ya virusi vya HIV wiki iliyopita.