Rais William Ruto leo Jumanne ataongoza Wakenya kusherehekea siku kuu ya kitaifa ya Utamaduni katika ukumbi wa Bomas jijini Nairobi.
Kauli mbiu ya sherehe hiyo mwaka huu ni “kusherehekea Umoja wetu kupitia utofauti wetu”.
Katibu katika Idara ya Utamaduni na Turathi za Kitaifa Ummi Bashir, amesema hafla tano muhimu zitaandaliwa katika sherehe ya mwaka huu.
Hafla hizo ni pamoja na maonyesho ya sanaa, vyakula vya kitamaduni, nyimbo za kitamaduni, michezo ya kuigiza, masimulizi ya kihistoria na maonyesho kuhusu desturi za jamii mbalimbali nchini.
“Katika sherehe ya mwaka huu ya utamaduni, tutakuwa na maonyesho ambayo hayajawahi kuwepo kuhusu tamaduni zetu mbalimbali,”alisema Bashir.
Awali, siku hii ilifahamika kama “Moi Day” hadi mwaka 2020 ilipobadilishwa jina na kuwa siku ya Utamaduni.