Kampuni ya umeme nchini, Kenya Power imetangaza kuwa mfumo wake una matatizo yaliyotokana na hitilafu ya mtandao kutoka kwa mtoa huduma wake.
Kutokana na hilo, kampuni hiyo imewataarifu wateja kwamba hawawezi wakapata baadhi ya huduma kama vile kulipia umeme kupitia kwa njia ya M-Pesa au USSD Code *977#.
Hata hivyo, Kenya Power inasema wateja wanaweza wakalipia umeme kupitia kwenye kumbi zao za benki, Airtel Money na benki zilizoidhinishwa.
“Tunafanya kazi na watoa huduma wetu kurejesha huduma zilizoathiriwa haraka iwezekanavyo,” ilisema kampuni hiyo katika taarifa leo Alhamisi na kuwaomba radhi wateja kutokana na hali hiyo.