Kazakhstan itaendelea kuimarisha ushirikiano wake na Kenya kupitia kutekelezwa kwa mkataba wa makubaliano, uliotiwa saini mwezi Mei mwaka huu kati ya Rais William Ruto na mwenzake wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev Jijini Astana.
Akizungumza Jijini Nairobi kwenye mkutano na wajasiriamali na wanahabari kabla ya kuadhimisha miaka 35 ya uhuru wa taifa hilo yatakayoandaliwa Jumapili, balozi wa Kazakhstan nchini Kenya, Barlybay Sadykov, alisema nchi hizo mbili tayari zimepiga hatua kubwa katika kutekeleza makubaliano hayo kwa manufaa ya raia wa nchi hizo mbili.
Kenya na Kazakhstan zilitia saini mikataba 10 ya maelewano wakati viongozi wa nchi hizo mbili walipokutana Jijini Astana mwezi Mei mwaka huu.
Makubalkiano hayo ni pamoja na uwekezaji, uchukuzi, uchimbaji madini, teknolojia ya habari na mawasiliano, na utalii.
“Tunataka kupeleka ushirikiano wetu katika viwango vya juu…..ushirikiano wetu katika uchumi wa biashara unazidi kustawi,” alisema balozi huyo.
Alidokeza kuwa maafisa wa serikali kutoka nchi hizo mbili, wamefanya ziara kwenye mataifa hayo ili kutekeleza mikataba iliyokubaliwa.