Shirika la Afya Duniani (WHO), limetangaza utumizi wa chanjo ya kukabiliana na virusi vya Ebola vilivyozuka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema walioshiriki kwenye matibabu hayo walipokea chanjo ya Ervebo katika eneo la Bunia, ambalo ni Makao Makuu ya mkoa wa Ituri, ulio Kaskazini Mashariki mwa DRC. Ugonjwa wa Ebola ulizuka katika mkoa huo wa Ituri.
Chanjo aina ya Ervebo, ambayo iliidhinishwa kukabiliana na aina ya Zaire ya ugonjwa wa Ebola, itatumika kikamilifu kwa matibabu ya binadamu kwenye majaribio ya kukabiliana na aina ya Bundibugyo ya virusi vya Ebola.
“Majaribio haya yatasaidia kuelewa ikiwa chanjo hiyo itafanikiwa kukabiliana na aina ya Bundibugyo,” alisema Ghebreyesus kupitia ukurasa wa X.
DRC imetangaza msambao huu wa 17 wa Ebola uliozuka mwezi Mei mwaka huu kuwa hatari zaidi, na umesababisha maafa 4,600 kati ya visa 9,700 ambavyo vimenakiliwa.