Washikili wa Kombe la Ligi ya mabingwa Afrika ,klabu ya Mamemolodi Sundowns walipigwa na butwaa baada ya kutemwa nje ya makala ya mwaka huu na limbukeni Wiliete Sports Club ya Angola, katika mchujo wa pili Ijumaa usiku.
Wiliete walifuzu kwa hatua ya makundi kwa mara ya kwanza kwa sheria ya bao la ugenini kufuatia sare ya bao moja mjini Pretoria katika mechi ya marudio baada ya duru ya kwanza kuishia sare tasa wiki jana.
Wiliete,iliyobuniwa mwaka 2018 itashiriki hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza .
Kwingineko Orlando Pirates pia ya Afrika Kusini iliwashinda wageni African Stars FC ya Namibia mabao 5-0, na kufuzu kwa hatua ya makundi kwa jumla ya ushindi wa 6-0 baada ya kushinda mkumbo wa kwanza goli moja bila ugenini.
Pirates wanarejea katika hatua ya makundi kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1995.