Kenya kuandaa kikao cha Michezo ya Jumuiya ya Madola

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya kwa mara ya kwanza imeteuliwa kuandaa kikao  cha michezo ya Jumuiya ya Madola, CGA kwa mataifa ya Afrika na yale ya Ulaya, tarehe saba na nane mwezi ujao katika kaunti ya Mombasa.

Kikao hicho kitaleta pamoja waakilishi kutoka zaidi ya mataifa 30 kutoka Ulaya na Afrika kusherehekea utamaduni wa Jumuiya ya Madola, kuimarisha ushirikiano na kupanga michezo ya Jumuiya ya Madola mwaka 2026 mjini Glascow, Scotland.

Mkutano huo utawashirikisha Marais wa mashirikisho ya michezo wanachama wa Jumuiya Madola miongoni mwa wengine.

Wao ni Rais wa Jumuiya ya Madola Chris Jenkins, Afisa Mkuu Mtendaji wa michezo ya Jumuiya ya Madola Katie Sadleir, Waziri wa Michezo Kipchumba Murkomen na Rais wa Kamati ya Olimpiki Kenya Dkt. Paul Tergat.

Share This Article