Kenya kuadhimisha siku ya Kifaru duniani kaunti ya Samburu

Tom Mathinji
1 Min Read
Kenya itaadhimisha siku ya Kifaru duniani kaunti ya Samburu.

Kenya itajiunga na ulimwengu Jumapili, kuadhimisha siku ya Kifaru duniani, sherehe hiyo ikiandaliwa katika hifadhi ya Sera kaunti ya Samburu.

Sherehe hiyo itakayoongozwa na waziri wa utalii na wanyamapori Rebecca Miano, inalenga kutoa hamasisho kuhusu uhifadhi wa vifaru.

Siku hii ya kimataifa ambayo iliadhimishwa mara ya kwanza mwaka 2011, inaangazia umuhimu wa kulinda aina tano  za vifaru ambao  ni  black rhino, white rhino, greater one-horned rhino, Javan rhino, na Sumatran rhino.

Aidha siku hii hutoa fursa kwa serikali, wahifadhi wa wanyamapori na wafadhili kushirikiana pamoja kuangazia hatari zinazokumba vifaru kama vile uwindaji haramu, kupotea kwa makazi yao na biashara haramu ya wanyamapori.

Kenya ina sababu maalum ya kuadhimisha siku hii, kutokana na idadi inayooongezeka ya vifaru hapa nchini.

Kenya pia ni nyumbani kwa aina mbili za vifaru waliosalia duniani northern white rhinos, ambao ni  Najin na Fatu, wanaoishi katika hifadhi ya Ol Pejeta.

Uhifadhi wa vifaru hapa nchini umeashiria ufanisi mkubwa kutoka na mikakati iliyowekwa ya kukabiliana na uwindaji haramu, uhifadhi wa mazingira wanamoishi na mipango ya kuwahamisha wanyama hao.

Maadhimisho hayo ya Jumapili yatasherehekea ufanisi huo, huku uhifadhi wa wanyama hao ukiendelea kupigiwa debe.

Share This Article