Kenya inakabiliwa na hatari ya kupokonywa fursa ya kuandaa fainali za mwaka ujao za Kombe la Bara Afrika (AFCON).
Kenya inatarajiwa kuandaa kipute hicho kwa pamoja na nchi jirani za Uganda na Tanzania.
Hata hivyo, inakabiliwa na hatari ya kupokonywa fursa hiyo endapo haitalipa shilingi bilioni 3.9 kwa CAF inavyohitajika kufikia mwishoni mwa mwezi huu.
Akizungumza jana Alhamisi alipofika mbele ya kamati ya bunge ya michezo, Katibu katika Wizara ya Michezo Elijah Mwangi alilitaka bunge kupitisha bajeti ya ziada ya shilingi bilioni 5 kwa maandalizi ya kipute cha AFCON.
Tayari waandalizi wenza Uganda na Tanzania wamelipa ada hiyo.
Morocco walikuwa wenyeji wa makala ya 35 mwaka uliopita.