Kampuni ya ndege ya Kenya Airways imesitisha safari zake kwa muda hadi visiwani Comoros na Mayotte ,kutokana na tahadhari iliyotolewa ya kuzuka kwa kimbunga cha CHIDO.
Kwa mjibu wa kampuni ya KQ hatua hiyo ni ya kuhakikisha usalama wa abiria na wafanyikazi wake.
Safari za kawaida zitarejelewa Jumatatu disemba 16 wakati ambapo hali ya anga inatarajiwa kuwa shwari.