China yatakiwa kuimarisha ushirikiano wake na Afrika

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto katika mkutano wa FOCAC nchini China.

Rais William Ruto, ametoa wito kwa China iimarishe ushirikiano baina yake na mataifa ya Afrika, kwa kusaidia mataifa hayo kupata ufadhili wa masharti nafuu kwa shughuli za maendeleo.

Rais aliitaka Uchina kushawishi wadau mbali mbali kuongeza maradufu michango yao kwa benki za maendeleo, kama vile chama cha kimataifa cha maendeleo ya benki ya dunia, ambazo hutoa mikopo ya riba nafuu kwa nchi zinazoendelea.

“Hatua hii itawezesha mataifa mengi ya Afrika kupata ufadhili. Itaunga mkono chumi ambazo zimeathiriwa zaidi,” alisema Rais Ruto.

Aidha alitoa wito kwa China kuunga mkono wito wa Afrika wa kuleta mabadiliko katika mfumo wa kimataifa wa fedha, alioutaja kutokuwa na usawa katika nchi nyingi, likiwemo bara Afrika.

Kiongozi wa taifa aliyasema hayo leo wakati wa mkutano wa uboreshaji barabara, ambao alikuwa mwenyekiti mwenza pamoja na naibu waziri mkuu wa China Ding Xuexiang, katika mkutano wa ushirikiano kati ya China na bara Afrika.

Wengine waliozungumza katika mkutano huo ni pamoja na Rais wa Gambia Adama , Lazarus Chakwera (Malawi), Brice Oligui Nguema (Gabon), Mohamed Younes Menti (Libya)  Al-Burhan Abdelrhman wa Sudan.

Website |  + posts
Share This Article