Kaunti ya Kiambu yazindua mpango wa maendeleo wa mwaka 2023-2027

Tom Mathinji
1 Min Read

Serikali ya Kaunti ya Kiambu imezindua mradi wa maendeleo utakaogharimu shilingi Bilioni 168.

Mradi huo wa maendeleo wa mwaka wa 2023 hadi mwaka 2027, uliozinduliwa na Gavana Kimani wa Matangi, unajumwisha miradi ya Afya, elimu, maji, barabara, Kilimo, nyumba za gharama ya bei nafuu na usajili wa ardhi kidijitali, miongoni mwa masuala mengine.

Kwenye mradi huo, Gavana Wamatangia meongoza makadirio ya bajeti ya miaka mitano kwa shilingi bilioni 52, huku akisema silingi bilioni 127.9 zitatoka kwenye mapato ya Kaunti na wahisani huku shilingi Bilioni 40 zikitokana na ushirikiano na serikali kuu, sekta ya kibinafsi na wahisani wengine.

Wamatangi amesema Kaunti hiyo inanuia kujiimarisha kimaendeleo kwa bajeti ya shilingi Bilioni 21.6, kila mwaka.

Sekta ya afya ambapo imekuwa ikishuhudia misongamano katika hospitali za kaunti hiyo, ukosefu wa vifaa na wafanyikazi wa kutosha, ina makadirio ya juu ya shilingi bilioni 40, hii ikiwa asilimia 26.

Mwenyekiti wa bajeti wa kaunti hiyo Josephine Nduta, alitoa wito kwa Gavana huyo kutekeleza miradi ambayo iliibuliwa na wakazi, akiongeza kuwa kamati ya bajeti imeidhinisha shilingi bilioni 22 kwa mwaka wa kifedha wa 2023-2024.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *