Katibu Omollo ahudhuria misa ya vikosi vya usalama

Marion Bosire
1 Min Read

Katibu wa usalama wa taifa Raymond Omollo alijiunga na maafisa wa vikosi mbali mbali vya usalama nchini kwa misa yao ya kila mwaka ya shukrani jana.

Misa hiyo katika kanisa katoliki ya Holy Family Minor Basilica jijini Nairobi ilihusisha maafisa wa huduma ya taifa ya polisi, maafisa wa magereza, maafisa wa kulinda wanyamapori, Wa kulinda misitu, maafisa wa huduma ya vijana kwa taifa pamoja na familia zao.

Omollo alipongeza maafisa hao kwa kujitolea kupambana na hali wanazokumbana nazo kazini.

“Kutafuta mwongozo wa Mungu na nguvu zake kazini na nyumbani ni muhimu kwa kila afisa wa usalama.” alisema katibu huyo huku akihakikishia maafisa hao uungwaji mkono kutoka kwa serikali, ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Website |  + posts
Share This Article