Katibu Mang’eni anusurika kwenye ajali Busia

Tom Mathinji
1 Min Read

Katibu katika Idara ya Biashara Ndogo na za Kati (MSMES) Susan Mang’eni, jana Jumatatu alihusika katika ajali ya barabarani katika barabara kuu ya Nambale-Korinda.

Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Bungeng’i  kilomita chache kutoka mji wa Busia, baada ya gari la Katibu huyo kugonga mwendesha pikipiki na kumuua papo hapo.

Katibu huyo alipelekwa hospitalini huku madaktari wakisema hali yake ni shwari.

Katibu Susan Mang'eni
Katibu Susan Mang’eni

Akithibitisha kisa hicho, Kamishna wa kaunti ya Busia Kipchumba Ruto alisema kutokana na ripoti ya polisi, gari la Mang’eni liligongana ana kwa ana na pikipiki.

“Tulipokea habari kwamba Katibu huyo alihusika katika ajali katika eneo la Bungengi kilomita chache kutoka mji wa Busia. Ajali hiyo ilisababisha kifo cha mwendesha pikipiki,” alisema Kipchumba.

Katika muda wa wiki mbili zilizopita, waendesha pikipiki watano wamefariki kupitia ajali za barabarani katika kaunti ya Busia.

Website |  + posts
Share This Article