Karua aongoza timu ya wanasheria wanaomtetea Besigye

Martin Mwanje
1 Min Read
Picha kwa hisani ya Nicholas Bamulanzeki

Mwanasheria wa Kenya Martha Karua ataongoza timu ya wanasheria watakaomwakilisha kiongozi wa upinzani wa Uganda Dkt. Kizza Besigye dhidi ya mashtaka yanayomkabili. 

Dkt.Besigye, pamoja na mshtakiwa mwenzake Hajji Obed, wanakabiliwa na mashtaka ya kumiliki silaha kinyume cha sheria na kuhatarisha usalama.

Wawili hao walifikishwa katika Mahakama ya Kijeshi ya Makindye iliyopo jijini Kampala leo Jumatatu.

Timu yake ya wanasheria inapambana aachiliwe kwa dhamana.

Dkt. Besigye alitekwa nyara wiki iliyopita na watu wasiojulikana wakati akihudhuria hafla ya uzinduzi wa kitabu kilichoandikwa na Karua chenye kichwa, “Against the Tide.”

Utekaji nyara huo umeshutumiwa vikali na viongozi wa upinzani nchini Kenya wakiongozwa na Kalonzo Musyoka na pia mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Juhudi za Dkt. Besigye kutaka kumwondoa Rais Yoweri Museveni madarakani zimekumbana na changamoto za kila aina, na mara kwa mara amejipata akikamatwa na wakati mwingine kujeruhiwa.

 

 

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *