Kanye West asema hakutaka kupata watoto na KimKardashian

Alisema hayo katika mahojiano na DJ Akademiks ambapo alilalamika kuhusu hali ngumu inayojiri katika mpangilio wa kusaidiana kulea watoto.

Marion Bosire
2 Min Read

Mwanamuziki wa Marekani Kanye West amesema kwamba hakutaka kupata watoto na Kim Kardashian, katika msururu wa semi zake za kusgangaza.

Akizungumza katika mahojiano na DJ Akademiks mwimbaji huyo alilalamika kuhusu hali ngumu inayojiri katika mpangilio wao wa kusaidiana kulea wanao wanne North, Saint, Chicago na Psalm.

Awali alilalamika mitandaoni kutokana na kile alichokitaja kuwa hatua ya mzazi mwenzake Kim ya kudhibiti visivyo wanao ambao anawarejelea kuwa wamarekani weusi.

Akademiks katika mahojiano hayo, alimuuliza Kanye kuhusu Kim na watoto wao wanne, ambapo alisema wengi wanahisi kwamba yeye ni kama huwa hawajibikii chaguo lake maishani hasa uhusiano uliozorota na mzazi mwenzake.

Ye alikubaliana na kauli hiyo na kuongeza kwamba makosa ni yake kwani hakutaka kupata watoto na Kim Kardashian baada ya miezi miwili ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi naye.

“Lakini hilo halikuwa mpango wa Mungu.” alisema Kanye.

Kanye West na Kim Kardashian walikuwa kwenye ndoa kwa miaka 6 kabla ya kutalikiana mwaka 2022.

Katika mahojiano hayo na Akademiks, Kanye alitetea chapisho lake kwenye mitandao ya kijamii kuhusu watoto wa Jay Z na Beyonce ambao alitilia shaka uwezo wao kiakili.

Alisema chapisho hilo ndilo bora ikilinganishwa na machapisho yake kuhusu Nazi.

Katika siku za hivi karibuni, Kanye amekuwa akifanya mambo kwa namna ambayo inashangaza wengi ambapo amekuwa akionyesha hadharani kwamba anaunga mkono Nazi na Adolf Hitler.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *