Kalonzo kuongoza ujumbe wa Azimio kwenye mazungumzo na Kenya Kwanza

Tom Mathinji
1 Min Read
Kiongozi wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka.

Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya, umezindua kundi la wanachama watano kuuuwakilisha kwenye mchakato wa mazugumzo na Kenya Kwanzaambayo yalipendekezwa.

Kwenye taarifa, Azimio walimtaja Kalonzo Musyoka kuwa kiongozi wa ujumbe huo.

Wanachama wengine ni kiongozi wa wachache bungeni Opiyo Wandayi, kiongozi wa chama cha DAP Eugene Wamalwa, seneta wa Nyamira Okon’go Omogeni, na mbunge wa Malindi Amina Mnyazi.

Muungano huo ulisema kwamba hakuna mrengo wowote utakaoshinikizia mwingine masuala ya kuwasilishwa kwenye kikao hicho cha mazungumzo.

Haya yanajiri baada ya Rais William Ruto kudokeza kwamba alifanya mazungumzo na kiongozi wa upinzani Raila Odinga,lengo likiwa ni kusitisha maandamano dhidi ya serikali yaliyokuwa yakishuhudiwa hapa nchini.

Rais alihakikisha kuwa, ghasia hazitakuwa sehemu ya siasa za taifa katika siku za usoni.

Baadhi ya masuala ambayo ujumbe wa Azimio unapania kuwasilisha ni pamoja na gharama ya juu ya maisha, ukaguzi wa matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 na kubuniwa upya kwa tume huru ya uchaguzi na mipaka, IEBC.

Mrengo huo pia unasema unataka kuwepo na makataa ya mazungumzo hayo ambayo yanafaa kung’oa nanga Jumanne, Agosti mosi,na kuendelea kwa muda wa mwezi mmoja.

Website |  + posts
Share This Article