Kalonzo awataka Wabunge wa upinzani kutwaa nafasi za wengi Jumanne

Kalonzo alisema haya alipofungua afisi za chama cha Wiper katika jitihada za kukipanua kujiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 ambao anatarajia kugombea urais.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kiongozi wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka, amewataka wabunge wa upinzani kutwaa nafasi za walio wengi wakati bunge litakaporejelea vikao Jumanne ijayo, Februari 11.

Akizungumza eneo la Magaraini, Kalonzo amesema ni bayana kuwa muungano wa Kenya Kwanza haukupata viti vingi kisheria na kuwataka Wabunge wa Muungano wa Azimio kuchukua nafasi zao kwani ndio walio wengi kulingana na uamuzi wa Mahakama Kuu uliotolewa Ijumaa.

Kalonzo alisema haya alipofungua afisi za chama cha Wiper katika jitihada za kukipanua kujiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 ambao anatarajia kugombea urais.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *