‘Kalamwah’ kazaliwa

Marion Bosire
1 Min Read

Mchekeshaji Mulamwah ambaye jina lake halisi ni David Oyando na mpenzi wake Ruth K almaarufu Bestie wamejaliwa mwanao wa kwanza wa kiume ambaye ni mwana wa pili kwa upande wa Mulamwah.

Ana kifungua mimba, mtoto wa kike na Carol Sonnie ambaye walitengana.

Wawili hao waliokuwa wamejawa na furaha walitangaza ujio wa mwanao Jumamosi Februari 10, 2024 kupitia akaunti zao za Instagram.

Ruth aliandika, “Tangu nilipokupakata kwa mara ya kwanza nilijua wewe ndio umekuwa ukikosekana kwenye maisha yangu. Vidole vyako vidogo vikiwa vimeshika vyangu, pumzi yako na unavyoniangalia.”

Aliongeza kusema kwamba anasubiri kwa hamu kutengeneza kumbukumbu zaidi na mwanawe wakati akikua.

Tayari mtoto huyo ambaye jina lake ni Oyando Junior amefunguliwa akaunti ya Instagram kama ilivyo ada kwa watu maarufu.

Share This Article