Kakamega Homeboyz mabingwa wa kombe la MozzartBet mwaka 2023 baada ya kuilaza Tusker FC bao moja bila katika fainali iliyopigwa Jumamosi Alasiri uwanjani Kasarani.
Timu zote zilitoka sare kuanko kipindi cha kwanza kabla ya , Kevin Amwayi kupachika goli la pekeena la ushindi katika dakika ya 73 .
Homeboyz wametuzwa shilingi milioni mbili na kombe pamoja na tiketi ya kuiwakilisha Kenya katika mashindano ya kombe la shirikisho la soka Afrika msimu ujao kwa mara ya kwanza.