Junior Starlets yawasili Cameroon kupanda mchongoma

Kikosi cha Mildred Cheche ni sharti kisajili ushindi wa mabao 2-0, ili kufuzu kwa Kombe la Dunia nchini Morocco mwishoni mwa mwaka huu.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya kwa wasichana walio chini ya umri wa miaka 17, iliwasili mjini Yaounde, Cameroon, jana jioni kwa marudio ya raundi ya tatu kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji Jumapili hii.

Starlets wanaowania kushiriki kipute cha Kombe la Dunia kwa mara ya pili kwa  mpigo watakuwa na kibarua kigumu, baada ya kupoteza bao moja kwa bila wiki jana katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo.

Kikosi cha Mildred Cheche ni sharti kisajili ushindi wa mabao 2-0, ili kufuzu kwa Kombe la Dunia nchini Morocco mwishoni mwa mwaka huu.

Website |  + posts
Share This Article