Jopokazi la kitaifa la ugonjwa wa Ebola linaloshirikisha mashirika kadhaa limekutana mapema Jumatatu kutathmini mikakati iliyowekwa ya kukabiliana na ugonjwa.
Kikao hicho kilichoongozwa na Katibu wa afya ya Mary Muthoni, kiliangazia mikakati ya kutafuta hela,utekelezaji wa Karantini,mbinu za mawasiliano,ugavi na matumizi bora vifaa vya afya na ushirikiano na washirika wa kimaendeleo.
Wizara ya afya imewataka Wakenya kuwa watulivu na makini pamoja na kufuata mikakati iliyowekwa ya kukabiliana na maambukizi na kuzuia maambukizi zaidi.
Mkutano huo aidha ulihudhuriwa na mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) humu nchini Dkt.Neema Kimambo, mshirikishi wa ukanda wa mashariki mwa Afrika katika shirika la kuzuia magongwa (CDC), pamoja na mwenyekiti wa shirika la wadu na wafadhili wa maendeleo ya Afya (DPHK) Luigi D’Aquino, na mwakilishi wa Baraza la Magavana nchini .