Jopokazi la Ebola latathmini mikakati ya kukabili ugonjwa huo

Wizara ya afya imewataka Wakenya kuwa watulivu  na makini pamoja na kufuata mikakati iliyowekwa ya kukabiliana na maambukizi na kuzuia maambukizi zaidi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Jopokazi la kitaifa la ugonjwa wa Ebola linaloshirikisha mashirika kadhaa  limekutana mapema Jumatatu kutathmini mikakati  iliyowekwa ya kukabiliana na ugonjwa.

Kikao hicho kilichoongozwa na Katibu wa  afya ya Mary Muthoni, kiliangazia mikakati ya kutafuta hela,utekelezaji wa Karantini,mbinu za mawasiliano,ugavi  na matumizi bora vifaa vya afya na ushirikiano na washirika wa kimaendeleo.

Wizara ya afya imewataka Wakenya kuwa watulivu  na makini pamoja na kufuata mikakati iliyowekwa ya kukabiliana na maambukizi na kuzuia maambukizi zaidi.

Mkutano huo aidha ulihudhuriwa na mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) humu nchini  Dkt.Neema Kimambo, mshirikishi wa ukanda wa mashariki mwa Afrika katika shirika la  kuzuia magongwa (CDC), pamoja na mwenyekiti wa shirika la wadu na wafadhili wa maendeleo ya Afya (DPHK) Luigi D’Aquino, na mwakilishi wa Baraza la Magavana nchini .

TAGGED:
Share This Article