Zaidi ya wanafunzi nusu milioni waanza mtihani wa kitaifa UCE nchini Uganda

UNEB imeonya dhidi ya kujihusisha na visa vya udanganyifu huku watu sita wakitiwa mbaroni kwa kujihusisha na uovu huo.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wanafunzi 503,055 wameanza mtihani wa kitaifa kidato cha nne (UCE) mapema Jumatatu katika vituo 4,514,ikiwa ongezeko ya asilimia 16.4 ya vituo 432,165, vilivyotumika mwaka jana.

Wanafunzi wameanza kwa mtihani wa somo la Hisabati na Kemia karatasi za kwanza.

Bodi ya mitihani nchini humo UNEB pia inaandaa mitahani ya wanafunzi 906 ya wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Wanafunzi wa kike wanaokalia mtihani huo ni wengi kuliko wale wa kiume ambapo  kuna wasichana ni 264,722 ikiwa asilimia 52.7, ya idadi yote ya watatahiniwa huku wanaume wakiwa 238,333 ikiwa asilimia 47.3.

UNEB imeonya dhidi ya kujihusisha na visa vya udanganyifu huku watu sita wakitiwa mbaroni kwa kujihusisha na uovu huo.

TAGGED:
Share This Article