Joho amkashifu Gachagua kwa kumtaka Noordin Haji ajiuzulu

Dismas Otuke
1 Min Read

Aliyekuwa Gavana wa Mombasa Hassan Joho amemkashifu vikali Naibu Rais Rigathi Gachagua kutokana na madai yake dhidi ya Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Taifa ya Ujasusi, NIS Noordin Haji.

Gachagua alitaja kuwa ofisi ya Haji imeshindwa kutekeleza majukumu yake katika hatua anayosema ilichangia maafa na uharibifu wa mali wakati maandamano ya Jumanne wiki hii.

Maandamano hayo ya kupinga Mswada wa Fedha 2024 yalifanyika katika maeneo mbalimbali kote nchini.

Joho amesema matamshi ya Naibu Rais yanasikitisha na yanaashiria kuwepo kwa mivutano katika serikali ya Kenya Kwanza.

Badala yake, Joho ametaka Rigathi kuwa katika mstari wa mbele na kujiulu kwanza badala ya kutaka watu wengine wajiuzulu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *