Angatua ya Jomo Kenyatta International Airport (JKIA),imetuzwa bora barani Afrika mwaka 2024 kwenye tuzo za World Travel Awards.
JKIA ilitawazwa bora baada ya kushinda angatua nyingine zikiwemo Cape Town International Airport ya Afrika Kusini,Casablanca Mohammed V International Airport nchini Morocco,Julius Nyerere International Airport nchini Tanzania,Kigali International Airport nchini Rwanda,King Shaka International Airport mjini Durban, Afrika Kusini na O.R. Tambo International Airport nchini Afrika Kusini.
Kaimu mkurugenzi Mkuu wa usimamizi wa viwanja wa ndege nchini Henry Ogoye alipokea tuzo hiyo katika hafla, iliyoandaliwa jana katika mkahawa wa Leisure Beach & Golf Resort huko Diani.