Japani watinga robo fainai ya Kombe la Dunia kwa wanawake baada ya kuwalabua Norway

Dismas Otuke
1 Min Read

Japani walijikatia tiketi kwa kwota fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuilabua Norway magoli matatu kwa moja katika mechi ya pili ya raundi ya 16 bora iliyochezwa Jumamosi nchini New Zealand.

Syrstad Engen alijifunga bao la dakika ya 15 kabla ya Guro Reiten kusawazisha dakiak 5 baadaye huku kipindi cha kwanza kikimalizika kwa sare ya bao moja.

Risa Shimizu na  Hinata Miyazawa waliongeza goli moja kila mmoja kunako kipindi cha pili kukamilisha ushindi huo wa Japani ambapo sasa watapambana na mshindi kati ya Uswidi na mabingwa watetezi Marekani katika hatua ya kwota fainali.

Website |  + posts
Share This Article