Anthony Otieno Ombok maarufu kama Jamal, alihifadhi bila kupingwa Urais wa shirikisho wa masumbwi nchini BFK, katika uchaguzi ulioandaliwa Jumamosi katika mkahawa wa Kasarani.
Maafisa 12 walichaguliwa bila kupingwa katika uchaguzi huo ambao ulihudhuriwa na msajili wa michezo nchini Roselyn Wasike kama mmoja wa wachunguzi.
Jamal atasaidiwa na Lydia Kinyua ambaye ni Naibu rais wa kwanza huku Chrispine Onyango akiwa naibu Rais wa pili.
David Munuhe Karitu, pia alirejea kama Katibu mkuu na atasaidiwa na Joseph Ochieng Otieno.
Benjamin Moses Oyombi pia alihifadhi wadhfa wa mtunza hazina na atasaidiwa na Gladys Musavi.
John Waweru Wangai pia alihifadhi kiti cha mratibu wa mashindano na atasaidiwa na Joselyn Mare.
Bondia mkongwe Ibrahim Wachira Bilali, na Dominic Opiyo were chosen as new members.
Viongozi waliochaguliwa watahudumu kwa kipindi cha miaka minne.