FKF yasaini makubaliano na Shirikisho la soka nchini Morocco kuimarisha soka

Dismas Otuke
1 Min Read

Shirikisho la soka nchini (FKF) limesaini mkataba wa maelewano na shirikisho la kandanda nchini Morocco (FRMF), kushirikiana katika mikakati ya kuimarisha soka humu nchini.

Mwafaka huo ulisainiwa jana jijini Rabat nchini Morocco baina ya kinara wa FKF Hussein Mohammed na mwenyeji wake kutoka FRMF Fouzi Lekjaa.

Kulingana na mwafaka huo, Kenya pia inatarajiwa kunufaika kutokana na maendeleo ya miundo mbinu ikiwemo viwanja na usimamizi wa shughuli za soka.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *