Tiketi za kombe la WAFCON zaanza kuuzwa

Mechi ya ufunguzi ya kipute hicho itasakatwa katika uwanja wa Olympic kati ya wenyeji Morocco na  Zambia Julai 5.

Dismas Otuke
1 Min Read

Tiketi za mashindano ya kombe la bara Afrika kwa wanawake  (WAFCON),  zimeanza kuuzwa Jumatatu ,ikiwa chini ya wiki mbili kabla ya kuanza kwa kipute hicho nchini Morocco.

Awamu ya kwanza ya tiketi itauzwa kuanzia Juni 26, kwa watumiaji wa kadi za VISA pekee,huku awamu ya pili ikifunguliwa Jumamosi hii Juni 28.

Mechi ya ufunguzi ya kipute hicho itasakatwa katika uwanja wa Olympic kati ya wenyeji Morocco na  Zambia Julai 5.

Kundi A linajumuisha wenyeji Morocco, Zambia, Senegal, na DRC, huku kundi B, likiwa na Nigeria, Tunisia, Algeria na Botswana

Kundi C linasheheni Afrika Kusini,Ghana, Mali, Tanzania.

Website |  + posts
Share This Article