Jaji Mkuu Mstaafu alalamikia madai ya utekaji nyara

Martin Mwanje
1 Min Read

Jaji Mkuu Mstaafu Dkt. Willy Mutunga amelalamikia madai yaliyokithiri ya kutekwa nyara kwa baadhi ya wanaharakati na waandamanaji wanaopinga Mswada wa Fedha 2024. 

Ametaja hatua hiyo kuwa kinyume cha sheria.

Akizungumza alipofika katika makao makuu ya idara ya upelelezi wa jinai, DCI leo Jumatatu, Dkt. Mutunga ametaka maafisa wa usalama kujiepusha na tabia ya kuwateka nyara raia akisema kila Mkenya anapaswa kujihisi huru kuishi humu nchini.

“Utekanyi nyara ni kinyume cha katiba. Mbona tuhofu kuishi katika nchi yetu?” Aliuliza Dkt. Mutunga alipofika katika makao makuu ya DCI akiwa ameandamana na wanaharakati kadhaa miongoni mwao Boniface Mwangi kuwasilisha malalamishi yao dhidi ya hulka hiyo.

Maafisa wa polisi wametuhumiwa kwa kuwalenga na kuwateka nyara watu wanaoonekana kupinga Mswada wa Fedha 2024.

Mwanablogu Billy Simani almaarufu Crazy Nairobian ni miongoni mwa watu walioripotiwa kutekwa nyara kabla ya kuachiliwa huru baadaye baada ya Wakenya kupaza sauti za kutaka aachiliwe.

Uongozi wa polisi haujatoa taarifa ya kina kuhusiana na madai hayo.

 

 

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *