Inspekta wa polisi afungwa miaka miwili jela kwa kushiriki ufisadi

Tom Mathinji
1 Min Read
Inspekta wa polisi Susan Wambui Muiruri ahukumiwa miaka miwili gerezani kwa kupokea hongo.

Afisa wa polisi anayesimamia kituo kidogo cha polisi cha  Zimmerman Susan Wambui Muiruri, amehukumiwa miaka miwili gerezani au alipe faini ya shilingi 650,000 kwa kushiriki ufisadi.

Alipofika mbele ya hakimu Isabella Baraza katika mahakama ya kushughulikia kesi za ufisadi za Milimani, Inspekta huyo wa polisi alitozwa faini ya shilingo 300,000 au kifungo cha mwaka mmoja gerezani katika kosa la kwanza na hukumu sawia na hilo katika kosa la pili.

Inspekta Wambui alipatikana na hatia ya kuwazuilia washukiwa katika kituo cha polisi kinyume cha sheria.

Uchunguzi ulibainisha kuwa afisa huyo alikuwa ameitisha hongo ya shilingi 10,000 ili kufanikisha majadiliano kati ya mlalamishi na washukiwa waliokuwa katika korokoro za kituo hicho cha polisi.

Hata hivyo washukiwa hao walilazimika kulipa shilingi 150,000 ambazo hawakufahamishwa na afisa huyo zilikuwa za nini.

Tume ya Maadili na Kupambana na ufisadi, imetoa wito kwa watumishi wa umma kukoma kushiriki kwa aina zozote za ufisadi na badala yake kuwatumikia wananchi kwa uadilifu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *