Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC imewataka maafisa wake kuwajibika katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Akizungumza Jumatano katika kaunti ya Mombasa wakati wa mafunzo kuhusu usajili wa wapiga kura, Naibu Mwenyekiti Fahima Araphat aliwataka maafisa hao kutumia vyema ujuzi waliopokea ili kuimarisha utekelezaji wa awamu ya pili ya usajili wa wapiga kura (ECVR ll).
Aliahidi kuwa tume hiyo itatafuta hela na rasilimali za kutosha kuanzisha awamu mpya ya usajili wa wapiga kura ikilinganishwa na ile ya kwanza (ECVR I).