Rwanda yaibwaga Congo na kudumisha rekodi ya asilimia 100

Katika matokeo mengine Algeria pia imeilaza Burundi seti 3-0 za 25-18, 25-13 na 25-18, katika uwanja wa Kasarani,pia ikiwa mechi ya kundi D.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rwanda imedumisha rekodi ya asilimia 100 baada ya kuwalemea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo seti 3-0, katika mechi ya pili ya kundi D, kuwania mashindano ya Voliboli Afrika, kwa wanawake iliyopigwa Jumatano uwanjani Kasarani.

Rwanda waliokuwa wameicharaza Algeria seti 3-0, katika mchauno wa ufunguzi wamepata ushindi dhidi ya Congo kwa seti za 25-17, 25-15 na 25-16, wakijivunia kutopoteza seti yoyote hadi sasa.

Katika matokeo mengine Algeria pia imeilaza Burundi seti 3-0 za 25-18, 25-13 na 25-18, katika uwanja wa Kasarani,pia ikiwa mechi ya kundi D.

Mashindano hayo yatakamilika Septemba 5 huku mabingwa wakifuzu kwa mashindano ya Dunia mwakani.

Share This Article