Serikali yalipa fidia ya bilioni 2.6 kwa familia 13,000 zilizotimuliwa Mau

Rais William Ruto ameoongoza utoaji wa shilingi laki mbili kwa kila familia iliyoathiriwa huko Sogoo, eneo bunge la Narok Kusini.

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali imelipa shilingi bilioni 2.6 kwa familia 13,000 zilizofurushwa kutoka msitu wa Mau katika kaunti ya Narok miaka sita iliyopita.

Rais William Ruto akiwa katika siku ya mwisho ya ziara yake katika kaunti ya Narok siku ya Jumatano, ameongoza utoaji wa shilingi laki mbili kwa kila familia iliyoathiriwa huko Sogoo eneo bunge la Narok Kusini.

Rais alisema kuwa serikali mnamo mwaka 2023 ilitoa fidia ya shilingi laki tatu kwa kila familia kwa familia zote 2,000 zilizokuwa zinaishi kwa mahema katika msitu wa Mau ili ziondoke katika eneo la chemchemi ya maji na kutafuta makao kwingineko.

“Leo tunafunga rasmi safari hii ndefu na yenye maumivu mengi kuhusu watu waliotiumuliwa katika msitu wa Mau, ambao sasa utasimamiwa na kaunti ya Narok,” alisema Rais.

Awali, Ruto alizuru na kukagua miradi kadhaa ya maendeleo katika eneo bunge la Emurua Dikirr, ikiwemo ujenzi wa soko la kisasa.

Share This Article