Timu saba za Afrika zaingia raundi ya 32 bora Kombe la Dunia

Pia upo uwezekano  wa timu mbili zaidi za Afrika kufuzu kwa raundi ya 32, bora endapo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo  na Algeria watajikatia tiketi mapema Jumapili.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu saba za Afrika kati ya kumi zimefuzu kwa hatua ya 32 bora katika makala ya 23, ya patashika ya Kombe la Dunia yanayoendelea nchini Marekani,Canada na Mexico.

Afrika imenufaika pakubwa kutokana na kuongezwa kwa idadi ya timu kutoka 32 hadi 48, ambapo jumla ya timu 10 zilifuzu kwa kipute cha mwaka huu.

Pia upo uwezekano  wa timu mbili zaidi za Afrika kufuzu kwa raundi ya 32, bora endapo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo  na Algeria, watajikatia tiketi mapema Jumapili.

DR Congo watakabiliana na Uzbekistan, ambao tayari wameyaaga mashindano katika pambano la mwisho kundini K,uwanjani Atlanta ,Chui wa Congo, wakihitaji ushindi uli kufuzu kwa raundi ya mwondoano.

Ghana ambao tayari wamefuzu watacheza dhidi ya Croatia, katika kundi L huku Uingereza, wakiwa na miadi na Panama, kuanzia saa sita usiku wa manane.

Share This Article