IEBC: Wapiga kura wapya 90,020 wamesajiliwa kwenye zoezi linaloendelea

Tom Mathinji
1 Min Read
Wakenya 90,020 wamesajiliwa kuwa wapiga kura kwenye zoezi linaloendelea la usajili wa wapiga kura kote nchini.

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), imesema kuwa wakenya 90,020 wamesajiliwa kuwa wapiga kura, kwenye zoezi linaloendelea la usajili wa wapiga kura lililoanza  Septemba 29, 2025.

Kwenye ripoti ya tume hiyo kuhuusu zoezi hilo, kaunti za Nairobi, Kiambu na Machakos zimeongoza kwa usajili huo zikisajili wapiga kura wapya 16,512, 9,917 na 4,026 mtawalia.

Kufikia Oktoba 31,2025,  wapiga kura 15,619 walikuwa wamehamisha vituo vyao vya kupigia kura, huku wapiga kura wengine 188 wakifanyia mabadiliko maelezo yao.

Nairobi, Mombasa na Kiambu pia zinaongoza kwa idadi ya wapiga kura waliobadilisha vituo vya kupigia kura ambapo wapiga kura 5,388, 1,791 na 1,766 mtawalia wamebadilisha vituo.

Kaunti zilizosajili wapiga kura wachache mno ni pamoja na  Tana River 130, Marsabit 284 na Isiolo 312. Tume ya IEBC inalenga kuwasajili wapiga kura wapya wapatao milioni 6.3 kabla ya uchaguzi mkuu wa mwka 2027.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article